Monday, March 30, 2009

Hivi ni kweli kuwa akitereza basi hatoacha

Hivi ni kweli kuwa akitereza basi hatoacha?


"Naona kama ina ukweli mkubwa sana kwani mimi mme wangu amewahi kucheat na nikamkamata lakini alitubu. Sasa naona tena dalili. Na katika kusomasome nimekutana na hii.

If a guy cheats on you, He'll do it again. If you stay, he'll cheat even more No woman can make a guy stop cheating, not even his mother. Cheaters are like a small kid, once they tasted sweets, no matter what you do or say, they'll find a way to get hold of them. Stop looking for water in a desert, because you'll find none.


Advice: Leave the looser and find a real man who'll give you his all OR stay with the cheat and be a subscriber of Kleenex Tissues, cos you will be weeping till you get to your grave. He might even find a girl to replace you, cos he doesn't really need you, or he'll keep you to cook for him and do his laundry, while he gets his groove on.

YAANI, HAPA NAHISI KAMA MIMI VILE!"

Jawabu:Sehemu pekee yenye ukweli ni "no woman can make a guy stop cheating" hata kwa upande wa pili hakuna mwanaume anaeweza kumfanya mwanamke aache kutereza. Whoever wrote this ni feminist na ana hasira, machungu na chuki dhidi ya wanaume kitu ambacho wanaume pia wanaandika kuhusu wanawake.


Watu wa namna hii huwa rahisi sana ku-turn kuwa players 4 life au watu wa ngono bila uhusiano hawajiiti machangudoa lakini wako radhi kufanya ngono bila kuhusisha hisia, labda kwa vile hawalipwi ndio maana hawataki kuitwa CDs.

Hii ni kwa vile wanakuwa wamekata tamaa kama sio kuogopa kuumizwa tena na jinsia hiyo kwani wanachukulia kila mwanamke/mwanaume anatabia hiyo hivyo ni bora kuwa na mtu kama yeye.

Kama mwanaume hajakuoa au hamko kwenye uhusianoa ambao ni committed hata mimi nitakushauri uanze mbele ikiwa mpenzi wako atatereza, lakini hadithi iko tofauti kwa wachumba, mume/mke kwani mpaka mtu anatereza lazima kuna walakini kwenye uhusiano hivyo badala ya kumuacha mwenza wako ni bora kutafuta ukweli wa nini hasa kimepungua/kosekana kwenye uhusiano wenu mpaka achomoke??!!


Kufanya mikakati kwa kushirikiana na yeye kukubali kosa na wewe kuwa tayari kumsamehe na kusahau (japo inachukua muda mrefu), mwenza wako kugundua nini alikuwa anakunyima na yeye kurekebisha ni wazi kuwa itafanya uhusiano wenu kuwa mzuri, Imara na wenye afya kuliko hapo awali.


Sikutumi utereze ili kuboresha uhusiano, la hasha!
Ninachojaribu kusema ahapa ni kuwa mwenza wako akifanya kosa la kusaliti ndoa/penzi haina maana kuwa ndio basi tena.....siku zote kuna njia ya kufikia muafaka.


Kama wapenzi mkachukua tahadhali mapema, mkajuana vema, mkaafikiana kushurikiana kwenye kila kona na mkawa wazi na kufanyia kazi uhusiano wenu badala ya kuachia "tunapendana" peke yake.


Unajua uhusiano ni kama ajira yenu ya pili, usipokuwa na bidii au kutokuwa makini ni wazi kuwa kibarua kitaota majani na mmoja wenu kutoka kwenye uhusiano 4 good au kutereza. Hivyo basi mimi sikubalini kabisa kuwa mwanaume au hata mwanamke akitereza basi ndio anakuwa wa kutereza unless kama ni hulka yake.


Vinginevyo ikitokea hiyo na mnapendana basi pigania penzi lenu na kulifanya liwe lenye afya na bora zaidi ya mwanzo.....kuweka "rules" kwenye uhusiano pale mmoja anapokuwa mtivu wa nidhamu ni muhimu.......wakati mwingine watu wanakuwa kama watoto, wanahitaji muongozo kutoka kwa mama.

Usiamini ktk ufeminist tafadhali, ni hatari kwa afya yako ya kimapenzi na Ngono.

Mwanaume na Mwanamke, nani anamuhitaji mwenzie?

Ndoa na Kuzaa

Sababu za Kusaliti Pendo

Dalili kuwa mpenzi anatereza

Dalili za Uhusiano Unaoharibika

Yale yanayoweza kuharibu ndoa!

penzi ni nini hasa

Misingi ya Uhusiano wa Kimapenzi

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment