Mke wangu akerwa na Kitumbo.....
"Nina ndoa yangu kwa miaka sita sasa tuna mtoto mmoja na tunategemea mwingine Mungu akijaalia mwaka huu. Baada ya uja uzito wa kwanza tumbo la mke wangu halikurudi katika hali ya mwanzo, yaani alikuwa na kitumbo kinamna fulani. Lilipungua lakini si katika hali ya mwanzo au tuseme ya kawaida.Tumejaribu kutafuta tight ya tumbo lakini haikusaidia, ingawa labda haikuwa nzuri sana.
Sasa tukafikiri na kuona labda kabla hajajifungua safari hii tujaribu kupata utaalamu wa jinsi gani tunaweza kupunguza na ikiwezekana kurudisha tumbo lake katika hali ya kawaida, maana hata yeye mwenyewe inamnyima raha kiaina. Sasa ni njia gani nzuri za kutumia zisizokuwa na madhara kwa afya? "
Jibu: Napata matumaini kuona kuwa wewe mwanaume unaungana na tatizo linalo mkera mkeo na kutafuta namna ya kumsaidia ili ajisikie anavutia tena baada ya kujifungua (wanawake wengi hujihisi kuwa hawavutii tena) kitu ambacho ni muhimu ili kumrudishia Mkeo kujiamini kwake akiwa mtupu hali itakayo pelekea ninyi wawili mfurahie miili yenu kwa uhuru zaidi.
Upangiliaji wa mlo (diet) na mazoezi kwa ruhusa ya Dakitari wake ni muhimu kutegemeana na alivyojifungua kwamba amejifungua kwa kawaida (asilia) au kwa upasuaji.
Pamoja na kuwa kufanya mazoezi kuna-sound rahisi mama wengi hushishwa kuyafanya kutokana na uchovu au kuwa na shughuli nyingi zinazohusiana na swala zima la kuwa mama.
Kabla hajaanza mazoezi ya kupunguza na kulikaza tumbo lake baada ya kujifungua atapaswa kulifunga (kiasili) na vilevile kujitahidi kupunguza unene ulioongezeka kutokana na ujauzito na anaweza kufanya hivyo kwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kutembea haraka-haraka n.k alafu baada ya kupunguza unene ndio afanye mazoezi ya tumbo.
Ngono baada ya kujifungua
Jinsi ya Kungonoana kwenye Ujauzito
Sunday, March 29, 2009
Mke wangu akerwa na Kitumbo.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment