Tuesday, March 31, 2009

Pesa anazo lakini hanihusishi

Pesa anazo lakini hanihusishi

Pesa kwenye mahusiano ya kimapenzi


"Mimi ni mwanamke wa 25 nimeolewa miaka 3 iliyopita kwa sasa ni mjamzito hivyo niliacha kwenda kazini tangu mimba hii ilipoingia kutokana na matatito ya kiafya. Mume wangu ana nafasi nzuri kazini na kipato chake kinakidhi mahitaji ya familia yetu.


Baada ya matumizi muhimu kwa kawaida najua anabakisha kama laki 5 kila mwezi lakini hakuwahi kunijulisha kama ana pesa hizo au ana plan gani na mabaki hayo ya pesa, nikimuuliza anasema hana pesa.


Wakati huo mimi kuwa baada ya mahitaji muhimu najua pesa fulani hubaki na sasa amefikisha million 5 lakini hataki kusema ukweli, Pesa hizo zipo kwenye account nami najua password yake lakini yeye hatambui hilo.
Je mtu wa design hii nimchukulie kama alivyo au nimweleze ukweli"


Jawabu: Asante kwa ushirikiano wako, inaonyesha wewe ni mmoja kati ya wanawake wachache ambae ulikuwa ukijituma ili kuchangia kipato ndani ya nyumba na ninachokiona hapa ni ile hali ya "kujishitukia" kwa vile hufanyi kazi unafikiri mume wako atakunyanyasa na bila kujijua unaamua kuomba pesa ambazo pengine wala huzihitaji....kama ulivyosema mwenyewe kuwa anakamilisha mahitaji yote muhimu.


Kitu kingine ninachokionahapa ni kuwa na hofu kuwa anaweza kuwa anazitumia pesa zinazobaki kwa ajili ya mambo mengine kama vile "kuwekeza" kwenye Ulevi na wanawake nje ya ndoa yane kwa vile tu wewe ni mjamzito (kutokana na matatizo ya kiafya ni wazi kuwa tendo la ndoa halipo vile inavyotakiwa kitu ambacho kinaongeza hofu).


Lakini kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa pesa zote zinazobaki baada ya mahitaji muhimu anazitunza Benk, hazitumii kivingine. Kumbuka wewe ni mjamzito which means kuna "mtu" mwingine ataongezeka kwenye familia yenu ndogo na badala ya kuwa wawili mtakuwa watatu nahivyo basi majukumu yataongezeka na kwa mshahara wa mtu mmoja tu mtoto hatokuwa na maisha bore.


Sasa ili mtoto kuwa na maisha bora au angalau "comfortable" ni wazi kuwa kuna ulazima wa ninyi kama wazazi kujiandaa na jukumu hilo jipya. Si hivyo tu bali kuna matukio ambayo hujitokeza bila mipango kama sehemu ya maisha yetu yanaitwa "udhuru" ni wazi kwa akiba inahitajika incase kitu kama hicho kinaibuka.


Sote tunapokuwa na mipango fulani na pesa tunazotunza ili kukamilisha jambo fulani alafu mtu akaibuka na kukuomba seti au kukuazima ni wazi kuwa utamwambia kuwa huna pesa....sio huna kabisaaa bali ulizonazo zinamipango yake muhimu na hutaki kuzigusa unless upate "udhuru" kama kuuguliwa, msiba n.k.


Umchukuliaje?-Since unalo neno/namba ya siri ya Benki Akaunti basi mchukulie kuwa ni mmoja kati ya mwanaume wachache wanaojua majukumu yao, anangalia mbele na sio pale mlipo (kuvaa miwani ya mbao) pia ni muaminifu na ndio maana akakupa neno/namba ya siri ya account (natumai hukuitafuta mwenyewe balia likupa baada ya kuomba).....vinginevyo mume wako anajaribu kufanya mambo yake kama mwanaume na wewe unapaswa kumuamini.


Nini cha kufanya-Hakuna ukweli wa kumuambia hapo kwasababu moja, Pesa ni zake, Pili hazitumii bali ziko pale zimetulia, tatu wewe unataka pesa za nini wakati kila kitu unatimiziwa ndani ya nyumba?


Kama unawasiwasi sana na wewe ni mwanamke kamilifu na mke hivi sasa ni lazima ulifunzwa namna ya kupata unachotaka kutoka kwa mume wako kwa kutumia lugha ya kimapenzi (siwezi kusema hapa kwani kaka zangu wakijua hatutopata kitu), sasa tumia mbinu hiyo kwa mume wako na hakika atakueleza mipango yake kuhusu pesa hizo (akiba) na hapo utapata amani moyoni mwako.

Acha kujishitukia kwa vile umeacha kazi, jiamini hali itakayokusaidia kumuamini mume wako.
Kila la kheri.

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment