Friday, March 27, 2009

Somo la mapenzi

Somo la mapenzi

Hivi unajua kuwa watu tunatumia muda mwingi kufikiria kuhusu mahusiano? kwamba unatamani ungekuwa kwenye uhusiano ikiwa huna mwenza, ungekuwa nje ya uhusiano ulio nao kwa sasa kwa vile huna raha, ungebaki kwenye uhusiano uliouacha kwa sababu bado unampenda mpenzi wako au kuboresha uhusiano ulio nao ambao unaelekea kubaya.


Mahusiano yanachukua/gharimu sehemu kubwa sana ya muda na nguvu zetu, mahusiano ni muhimu ktk maisha yetu, mafanikio yetu, furaha/raha zenu. Mahusiano yanagusa kila kona ya maisha yetu kuanzia kazini, nyumbani, familia na mapenzi.

Uhusiano wenyewe una maana kuwepo pale kwa ajili ya mwenzio, kuchangia na kusheherekea undani wa furaha ya ajabu na ya kipekee mioyoni mwetu (nani anataka kuwa mpweke jamani eeeh?).


Nyumbani na kwenye familia uhusiano una maana kufurahia ukuaji wenu, ukaribu wenu, kupena matumaini, kukosoana, kurekebishana, ushirikiano wenu n.k.


Kazini/Shuleni uhusiano una maana kusaidiana, kurekebishana, kupena matumaini, kukosoana, kupongezana yanapookea mafanikio n.k.
Kwenye mapenzi uhusiano unamaana kusheherekea “u-mutual”(nipe- nikupe), kupeana mapenzi yasio na kikomo, kushirikiana kila kitu kuanzia mate mpaka miili yetu, kukosoana, saidiana, rekebishana, jifunza n.k.


Kitu kinachonigusa kuhusu mahusiano ni kuwa hatukufundishwa tulipokuwa shuleni japo kuwa tulihitaji sana kujua jinsi ya kuanzisha uhusiano mzuri na wa kudumu kwa muda mrefu ktk maisha yetu, yaani kama vile tulivyofundishwa Kiingereza, Hisabati, Historia, Sayansi, Sanaa na Michezo

penzi ni nini hasa

Misingi ya Uhusiano wa Kimapenzi

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment