Tuesday, March 17, 2009

Yale yanayoweza kuharibu ndoa!

Yale yanayoweza kuharibu ndoa!



Mimi ningependa kufichua yale ambayo wanaume tunayo, na kwa nini tunafanya hivyo. Kwa upande huo wa kutokuwasiliana, ipo dhana tumejijengea kuwa si vyema kumzoesha mkeo kila kitu, kwamba mimi nafanya hivi au nataka kufanya vile kwa mfano kukupigia simu mara kwa mara inaleta mazoea ambayo ukikosa kupigiwa utaleta dhana potofu, hii ni moja ya sababu.


Lakini ipo sababu kubwa ambayo hata nyie wanawake mnayo, ni ile ya kujisahau. Kwamba sinimeshaoa, sinimesha-olewa, kuna sababu gani ya kuhangaika mara simu mara nifanye hiki na kadhalika.


Wengi wanasema eti mkishaoana, mnazoeana kama dada na kaka. Wewe dada ni dada na mke au mume ni hivyo hivyo, havina mbadala. Jiulize kama ni dada yako unaweza ukaoga nae? Kwa hiyo kila siku inapokwenda hakikisha unajiweka kama vile `unatafuta’.


Kila siku inapokwenda hakikisha hufanyi makosa ya kumfanya mwenzako ahamanike ni `vipita njia’ kwani jamani kila kukicha vinazaliwa vyombo…. Kwa hiyo hasa kwa hawa wanaosafiri hukutana ni vishawishi hivyo ambavyo vinawaweka njia panda.


Jingine la muhimi ni mawasiliano. Hili ni tatizo, sugu,sisemi mawasiliano ya simu,nasema mawasiliana kama mke na mume. Sisi wanaume mara nyingi hatupendi kujadilia, hasa katika maswala ya ndani, ya kimahusiano, tunataka kufanya.


Mnapokuwa ndani mjaribi kujadili, kuelezena na kupeana ushauri kuhusu hili au lile. Nashangaa wengine wanasema maswala ya mapenzi hayahitajiki majadiliano mkiwa mumeshaoana,kwanii mnatafute nini zaidi! Inabidi tujadili, tuelekezaneni ka kuwekana sawa.

Unaacha bwana au bibi keshasafiri unaanza kulalamika huku nyuma. Pale mkiwa uso kwa uso ndipo pa kujadili. Mhh, yapo mengi ngoja niwaachie wenzangu, wenye nia ya kufichua uzaifu huu, ili tujenge mahusiano mema."

Nafichua, machache ya wanawake ambayo yanaweza kuharibu ndoa;

(1)-Kufunga ndoa bila kuwa tayari (kufuata mkumbo, kuamini ni baraka, kufuata pesa).

(2)-Wanawake tukipenda na kupendwa huwa na tabia ya kujisahau pale tunapojuwa tumeolewa, u dont put an effort anymore kwa kuamini kuwa amekuoa so hawezi kwenda popote.

(3)-Kutokujua tofauti kati ya Mpenzi na uhusiano......wengi hutegemea "hisia" kuboresha penzi hawajui kuwa unatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwa na uhusiano udumu.

(4)-Kukimbilia kuzaa (kwa imani kuwa ni kukoleza mapenzi) bila kuwa tayari/kujua utajigawa vipi kati ya mapenzi, uhusiano na majukumu kama mama.

(5)-Kumtegemea mwanaume kwa kila kitu yaani kumfanya "ajira".

(6)-Kujiachia kwa maana ya kutojipenda tena na una"tilia" vivazi vizuri ikiwa tu unakwenda kwenye sherehe au unakoga na kujifukiza manukato siku ukiwa unataka tendo.

(7)-Kuchukulia Ngono kama wajibu.......uvivu wa kujifunza kupenda tendo hilo takatifu.

(8)-Kuamini ktk msaidizi (houseBoy/Girl)......kumpikia mwanaume ni alama ya upendo (kule nitokako mimi) hivyo Vigoli huwa hatupikii wanaume ovyo-ovyo unless njemba kama imekuja kuchumbia.

(9)-Heshima ya uoga....huna mpango wa kumheshimu mume wako lakini unamuogopa au unaogopa kuachwa.

(10)-Kutokuwa na tabia ya kum-challenge mumeo, kila asemacho wewe ni "ndio bwana"...challenge him, onyesha kuwa u r smart woman!

(11)-Kutokumpa mume wako muda wa kutosha....unakuwa busy na marafiki/shoga au familia yako kila wiki.

(12)-Kujihusisha sana kwenye familia yake hasa kama kuna migogoro kati ya ndugu na ndugu. Unatakiwa kuwa upande wa mume wako lakini jua ur limit, kamwe usiponde ndugu zake hata kama yeye anawaponda.

(13)-Ile kaingia tu unamuwahi na nini kilitokea b4 hata hajanywa chai/kaa chini nakutuliza akili...hujui siku yake ilivyokuwa mama, ongea nae lugha ya mapenzi kumlainisha, mkande ili awe relaxed kabla hujamshitaki mwanao kuwa aligoma kwenda shule au kafeli jaribio la hisabati.

Yapo mengi ila kwa sasa wacha nitunze ndoa yangu.

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment