Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaume wanaoingia kwenye uhusiano  wa kimapenzi na kuoa kila siku ni wengi lakini je wanaoolewa wote  wanaingia kwenye maisha ya ndoa na watu sahihi? Jibu ni hapana, na hii  ni kwa sababu wanawake wengine wanakubali kuolewa na wanaume ambao  hawakujiandaa kuingia kwenye maisha hayo. Dalili zenyewe ni hizi hapa  chini.
Waliobaini kuwa ni muda mufaka
Unaweza  kuwa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye umri wake umekwenda lakini bado  anaona anastahili kuwa kwenye maisha ya ‘ubachela’. Ukikubali kuolewa  na mwanaume wa sampuli hii lazima atakusumbua lakini yule ambaye amekaa,  akatafakari kisha akagundua kuwa ni wakati muafaka wa kuoa, ni wazi  huyo atakuwa amejiandaa na hata ukimkubalia sidhani kama utajuta.
Anajiamini, siyo tegemezi
Ni  kweli mapenzi hayana uhusiano wowote na fedha lakini ukweli usiofichika  ni kwamba kama mwanaume hana kazi inayomuwezesha kumuingizia kipato,  hawezi kuwa miongoni mwa wale wanaostahili kuingia kwenye maisha ya  ndoa.
Ukikubali kuolewa na mwanaume asiye na kitu eti kwa sababu tu  umempenda na moyo wako hauko tayari kumkosa, ujue unajiingiza kwenye  maisha ya bahati nasibu kitu ambacho siyo kizuri. Kama huyo uliyenaye  siyo tegemezi, ni mtu mwenye uwezo wa kukulisha na kukutimizia shida  zako zinazohitaji fedha, usione hatari kumwambia afanye hima akatoe  mahari muoane.
Anachukua nafasi ya baba
Kuna  baadhi ya wanaume licha kwamba hawajaingia kwenye maisha ya ndoa na  hawajafanikiwa kuwa na watoto lakini wameshaanza kuzishika nafasi za  ‘ubaba’. Unaweza kuwa na mpenzi akawa ni mtu wa kupenda sana watoto na  wakati mwingine kuzungumzia namna wa kwake watakavyokuwa. Huyu ni  mwanaume ambaye ana dalili za kutaka kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Anakuchukulia kama mke wake
Chukulia  kwamba uko na mpenzi wako lakini jinsi anavyokuchukulia ni kama mke  wake. Kwa kifupi utaanza kumuona anachukua nafasi ya mume. Kwa mfano  ataanza kuweka mikakati kwa ajili ya maisha yenu ya baadae,  atakutambulisha kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, atakuwa  akikushirikisha katika kila suala linalogusa maisha yako na yake.
Aidha,  mtaalam wa masuala ya mapenzi nchini Marekani, Carol Morgan anaongeza  kuwa, licha ya yote hayo pia mwanaume huyo atakuwa ni mkweli na muwazi  katika kila jambo.
 Hizo ni dalili nne za mwanaume ambaye amejiandaa  kuingia katika maisha ya ndoa. 
No comments:
Post a Comment