Tunapozungumzia uhusiano wa kimapenzi, tunazungumzia watu kuwa pamoja  na kushirikiana katika kila jambo linalogusa maisha yao. Hata hivyo,  watu wanaweza kutokea kupendana lakini yakajitokeza mazingira ambayo  yanawalazimisha kuishi mbalimbali.
 
 Wapo waliooana lakini kazi au sababu nyingine zimewafanya waishi mbalimbali. 
Kuna wachumba na wapenzi wa kawaida ambao kutafuta maisha kama vile kazi na elimu vimewafanya waishi maeneo tofauti.
 Unakuta huyu yuko Tanga, mwingine yuko Arusha. Huyu yupo Tanzania  mwingine yuko Marekani lakini wanapendana na hakuna aliye tayari kumkosa  mwenzake.
Katika hili, ninachotaka kukizungumzia ni hii kasi ya wapenzi wanaoishi mbalimbali kusalitiana.
 Katika mapenzi ya kweli hakuna suala la kusalitiana, kila mmoja  atajitahidi kuvumilia na kuhakikisha anavishinda vishawishi ili asigawe  penzi kwa mtu mwingine.
Lakini sasa kuna mazingira flani ambayo  yakiwepo kusalitiana kunakuwa na asilimia kubwa kutokea. Juzi  nilibahatika kuzungumza na dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la  Fauzia.
 Yeye anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mchumba wake aliyemtaja kwa jina moja la Juma anasoma Uganda.
 Dada huyu anasema: “Tulikuwa tunapendana sana, alikuwa ananipa mapenzi  ambayo sijawahi kuyapata, aliniahidi ndoa akanivisha pete lakini huku  tunakoelekea naona kabisa hatutafikia ndoto zetu.
“Yeye yuko  Uganda na mimi niko Dar lakini taarifa niliyopewa na ndugu yangu aliyepo  chuoni hapo ambaye hawajuani ni kwamba, mchumba wangu huyu ana mtu  mwingine huko na wamekuwa wakionekana maeneo wakiponda raha.
 “Naumia sana kwani kila nikimpigia simu na kumuuliza juu ya hilo  ananiambia, hayo ni maneno ya watu wasiopenda kutuona tunapendana. Eti  ananiambia hana mwingne anayempenda zaidi yangu lakini huku naambiwa ana  mtu mwingine.”
Hilo limemtokea Fauzia lakini ninachoamini ni  kwamba hayo ndiyo mazingira yanayojitokeza kwa wapenzi wengi wanaoishi  mbalimbali. Uvumilivu na uzalendo vimekuwa vikiwashinda wengi.
 Mpenzi wako anaweza kuwa mbali na wewe na akakuahidi kutokukusaliti  lakini akiwa huko akakusaliti bila hata wewe kujua, lakini watu  wanaoujua uhusiano wenu wanabaki kukuonea huruma.
Ni suala  lisilo na ubishi kwamba hisia ni kitu kigumu sana kukizuia, unaweza  kumuuliza mtu kwamba, anawezaje kukabiliana na hisia zake wakati mpenzi  wake yuko mbali?
 Jibu atakuambia eti akijiwa na hisia hizo anajiweka bize na mambo mengine.
Ni kweli wapo wanaoweza kufanya hivyo lakini wengi wanaishia kusaliti tena wengine huku mioyo yao ikiwauma.
 Mioyo yao inawauma na roho zao zinawasuta kwa kuwa wameshawaahidi  wapenzi wao kuwa hawatawasaliti lakini wanafanya hivyo kwa sababu ya  tamaa zao.
 Usaliti unakujaje?
Kwanza ifahamike kwamba,  kama mpenzi wako yuko mbali sana na wewe na mnakaa kwa muda hata wa  miezi sita na zaidi bila kuonana, kusalitiwa kuna asilimia nyingi ila  unachotakiwa kukifanya ni kumuamini tu mpenzi wako.
Unatakiwa  kumuamini tu kwa kuwa, kwanza ni vigumu kubaini kuwa anakusaliti na hata  ukimuuliza atakuambia hawezi kukusaliti lakini kumbe inawezekana hata  muda huo wakati mnaongea yuko na mtu mwingine kitandani.
Iko hivi, kama mpenzi wako yuko masomoni, elewa huko aliko atakutana na mtu mwingne ambaye naye mpenzi wake hayuko naye.
 Hawa wataanzisha urafiki wa kwaida, watapeana kampani za hapa na pale  lakini hawa wanayo nafasi kubwa ya kuwasaliti wapenzi wao, na hiki  ndicho kinachotoea kwa wengi.
Hilo liko sana vyuoni na makazini  hivyo kama mpenzi wako yuko mbali na wewe kwa sababu ambazo  hazizuiliki, unatakiwa kuwa na moyo wa uvumilivu au utakiwa kuwa ni mtu  wa kupotezea sana laa sivyo unaweza kujikuta unaachana na mtu ambaye  ulitokea kumpenda sana.
Kujizuia ni vigumu?
Wapo wanaoweza  kukabiliana vilivyo na tamaa zao, hawa ni wale wachache wanaowaheshimu  wapenzi wao, wanaoweza kutafuta njia mbadala za kuziridhisha nafsi zao  pale hisia za kufanya mapenzi zinapowajia.
Saturday, March 17, 2012
Ukiwa mbali na mpenzi wako, mezea lakini jua unasalitiwa!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment