Tuesday, March 31, 2009

Naogopa Kungonoka baada ya kuzaa

Naogopa Kungonoka baada ya kuzaa

Ngono baada ya kujifungua

Jinsi ya Kungonoana kwenye Ujauzito


"Tatizo langu la kwanza ni kuhusu kuongezeka kwa mwili na nikijaribu kila njia ya kupunguza mwili lakini imeshindikana nisaidie dada nateseka maana hata umbo langu namba nane wanavyosema wabongo limeanza kupotea.Samahani kwa kujisifu kidogo maana sifa jipe mwenyewe ukisubiri kusifiwa hautompata hata mmoja siku hizi.


Pili mimi ni mama mwenye mtoto wa umri wa miezi sita tatizo langu siku hizi naogopa sana kufanya ngono na baba yake maana naogopa kunasa mimba na kumuharibu mtoto, lakini hamu nakuwa nayo mpaka inafikia wakati nafanya. Sasa naomba nisaidie njia nzuri ya kupanga uzazi maana nimesha ambiwa vidonge nilijaribu lakini vimenisababishia aleji na sasa sishiki vitu vya baridi nimeacha hivyo sina njia nyingine nimeambiwa kuna za kienyeji sijui hata moja nisaidie napata shida."

Jawabu-Asante ,Kuongezeka mwili baada ya kujifungua ni kawaida kwa baadhi ya wanawake na kupungua kwake sio ngumu sana japokuwa unahitaji kujituma kufanya mazoezi na kuangalia lishe yako (diet).


Kama ulivyosema wewe unaumbile la nambari nane ni wazi kuwa unanenepa zaidi makalio, mapaja na sehemu ya juu inaongezeka kidogo tu ili ku-balance umbile si ndio? Ukifanya "diet" ya kujinyima chakula au kuruka baadhi ya virutubisho unaweza kabisa kupungua mwili kwa kipindi kifupi sana lakini njia hiyo sio nzuri na inaweza kukusababishia matatizo ya kiafya hapo baadae na vilevile kubaki na minyama uzembe.


Njia nzuri ni kufanya mazoezi mepesi ili kupunguza uzito alafu kufanyia kazi/mazoezi maeneo ambayo wewe unadhani yamezidi unene na ungependa yapungue.....mfano tumbo, mapaja na mikono...hata kama una umbile la namba nane tumbo likiongezeka tu basi ule mkato wa kuifanya nane ionekane unapotea, pia unene/ukubwa wa mikono utakufanya uvae nguo kubwa ambazo ni wazi kuwa zitaziba/poteza umbile lako sehemu ya kifuani na tumboni, mapaja yakinenepa ni wazi yatakuwa yakisuguana na ili kuepuka hilo itakupasa uvalie nguo kubwa ili zisijisugue juu ya ngozi yako.


Lakini kama unene wako ni sehemu ya "side effects" za madawa ya kuzuia mimba ambayo umekili kuwa uliwhai kutumia kupungua unene inaweza kuwa mbinde kidogo, lakini kama unene wako ni kutokana na kujifungua/zaa basi hakuna matata ukijituma na kuwa na nia moja basi utafanikiwa.


Kwa kuanzia basi hakikisha unakula ili kutosheka na sio kushiba, ukihisi kutosheka basi acha kula hata kama chakula ni kitamu kuliko. Kula kwa wakati Mf-Kila baada ya masaa manne na hakikisha huli Chakula cha wanga masaa mawili kabla hujaenda kulala(kula mapema chakula cha jioni/usiku)......wekeza zaidi kwenye maji, matunda na mboga za majani kwenye kila mlo wako ili kuhakikisha unapata kishe kamili kila siku yenye virutubisho vyote muhimu.


Alafu sasa ndio unaweza ukaanza mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba nakutembea mwendo mrefu....hii itakusaidia kupunguza mwili na baada ya hapo sasa ndio utapaswa kuwa unafanya mazoezi hayo ya kawaida ukichanganya na yale tunayaita "shape up" ambayo hufanywa kwa kulenga maeneo fulani tu....


Uzuri wa kupunguza uzito/unene kwa kufanya mazoezi ni kuwa, misuli yako inakuwa imara na kukaza, tofauti na kupunguza uzito kwa kujinyima chakula.


Njia za uzazi za kienyeji- Hata mimi sizijui za kienyeji, najua mbili za kiasili ambazo ndio natumia nazo ni tarehe na kumwaga nje bila kusahau ya kisasa ambayo ni Condoms(wakati wa siku za hatari).....mbili za kiasili sio asilimia mia moja kama yalivyo madawa, akitereza kidogo tu kitu na box.....utahitaji sana ushirikiano wa mumeo hapo.


Condom ni the best way ya kuzuia mimba na haina madhara, sasa zipo bidhaa mpya ambazo hazisababishi madhara yeyote kwa watumiaji ambao awali walikuwa wakidhurika na bidhaa za mipira.....watembelee Dulex wanabidhaa bomba sana wale, tena kuna ndom nyingine zinaongeza utamu wa tendo na wala hatohisi kama kavaa kitu na huenda akapenda kuzitumia kuliko kufanya nyama 2 nyama.

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment