Thursday, March 15, 2012

Afya na Imani Kwa Mwanafunzi

Hakuna kitu kinachoitwa bahati katika maisha ya Kisayansi, isipokuwa yanayotokea hutengenezwa kupitia mawazo ya watu wenye fikra hasi na chanya. Kwa kuwa sisi ni wanafunzi ambao tunatarajia kupata mafanikio katika kusoma kwetu lazima tufahamu msingi mzima wa kuvuta kitu kinachoaminiwa kama BAHATI.

Siku zote IMANI ni kitu cha ajabu sana ambacho kwa miaka mingi kimewafanya wanasayansi na watafiti mbalimbali kukuna vichwa juu ya kitu hiki. Dunia imeshuhudia watu wakiamini juu ya mambo fulani na kupata matokeo halisi. Katika nchi yetu kuna watu wanaamini katika dini, mizimu na kadhalika.

Lakini ukweli unabaki kuwa wote kwa pamoja wanapata matokeo kwa sababu ya imani zao. Wenye kuomba mvua kwa matambiko wamekuwa wakifanikiwa na wa upande wa waomba Mungu nao kwa namna yao wamekuwa wakipata matokeo ya kushangaza, hali kadhalika wanaojiamini wenyewe wamekuwa wakishinda juu ya mambo kadhaa.

Hivi ndivyo ulimwengu wote kwa ujumla wake unavyoendeshwa na wanadamu. Swali linakuja Imani ni kitu gani na kina faida gani katika maisha ya mwanafunzi ambaye ndani ya kitabu hiki anazunguziwa kwa kina?

Ukweli ni kwamba IMANI ni sanaa inayojumuisha nguvu za kiroho ambazo mwili wa mwanadamu umeubwa nazo. Kama nilivyosema katika mada zilizopita kwamba mwili una uwezo wa kila namna, kinachokosekana kwa watu wengi ni ujuzi tu wa namna ya kuutumia mwili na kupata matokeo stahili ya maisha.

Mwili tunaweza kuufananisha na bunduki, akiwanayo anayefahamu kuitumia anaweza kufyatua risasi akaua, lakini kwa asiyekuwa mjuzi ataangamia licha ya kuwa na kitu chenye uwezo mkononi mwake.

Tunapozungumzia Imani katika maisha ya mwanafunzi tuna maanisha kwamba ili msomi avute kitu kinachoitwa bahati lazima aamini jambo moja tu nalo ni kufanikiwa katika masomo yake.

Mwanafunzi hatakiwa kuwa na majibu mawili anapofikiria mafanikio ya masomo yake, kwa lugha nyingine maisha ya mwanafunzi yanatakiwa yajae mawazo chanya au positive thinking kwa kiingereza.

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment