Thursday, March 15, 2012

Athari za Mwanafunzi Kufuata Ukumbi

Uchunguzi unaonyesha kwamba wanafunzi wengi hubadilika kitabia wanapokuwa masomoni. Hii ina maana kuwa wazazi wanaweza kujitahidi kumuandaa mtoto wao lakini wakajikuta wanapata matokea ambayo hawakuyatarajia.

Jambo kubwa ambalo huathiri tabia za wanafunzi wawapo shuleni ni kutekwa akili zao bila wao wenyewe kujua kwa kufuata tabia za kimakundi au kwa lugha ya kigeni Mob- psychology.

Inawezekana kabisa mwanafunzi akatoka nyumbani na kujiunga na shule fulani akiwa mtu safi mwenye akili darasani, lakini baadaye akajikuta anabadilika kidogo kidogo na kufikia hatua ya kuwa muhuni na hata mtumiaji wa dawa za kulevya na hatimaye kushindwa masomo.

Hivyo, ni wajibu wa mwanafunzi mwenyewe kuwa makini na mvuto wa kimakundi atakaoukuta shuleni na kujihadhari. Inashauriwa kuwa si busara kuiga kila jambo linalofanywa na wengine kwa msukumo wa nje, mfano kuona aibu kwa kuitwa mshamba.

Dondoo zifuatazo ni muhimu zikazingatiwa na mwanafunzi awapo shule ili aweze kuepukana na ushawishi wa kimakundi ambao wakati mwingine huharibu tabia ya mtu na kuleta madhara kwa muhusika na familia yake.

*Si vema kujiunga na makundi kufanya jambo fulani bila kutafakari kwa kina faida na hasara. Ni muhimu kwa mwanafunzi kusimamia jambo analoliamini na kutokukubali kubadilika kirahisi kwa kushawishiwa au kuzongwa na kauli za wengi.

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment