Imani nayo inapaswa iambatane na matendo ambayo yanaashiria kupiga hatua  kuelekea mafanikioni kwani imani yako ndiyo itakayokufikisha kwenye  kile unachokihitaji.
Hata kama wewe ni muumini mzuri wa dini,  lakini kama imani yako ni ndogo, si rahisi kujibiwa maombi yako kwani  unakuwa huamini kama kweli inawezekana.
Amini kuwa Mungu yupo na hashindwi kitu endapo kama utamuamini na kupanua imani yako kwake.
Uamuzi  wa maisha mazuri ya kesho uko mkononi mwako, kama unaishi maisha ya  taabu na mateso kwa sasa basi kuna mahali ulikosea huko nyuma. Huo ni  ukweli mtupu.
 Hakuna mtu anayeweza kukumulia maisha yako ya  kesho isipokuwa wewe mwenyewe. Achana na tabia ya utegemezi kwa wengine  na badala yake sasa anza kupigana wewe kama wewe.
Saturday, March 17, 2012
Hakuna Imani Bila Matendo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment