Katika maisha, hakuna kitu kinachoweza kufanyika kama hakutakuwa na bidii ya utendaji. 
Huo ndiyo ukweli, bidii ni kiungo muhimu sana katika kufanikisha jambo lolote kwa mtazamo chanya.
Lakini  bidii peke yake inatosha kukamilisha mafanikio maishani? Jibu ni kwamba  si kweli kwani pamoja na bidii kuwa kiungo muhimu cha mafanikio, lakini  bado kuna vitu vingine muhimu zaidi ili kujipatia maendeleo na  mafanikio maishani ambavyo ni Uaminifu, Ukweli na Imani.
Vitu  hivi kwa pamoja vinakamilisha nguzo kuu muhimu maishani kwa mtu  aliyedhamiria kupata mabadiliko. Katika kila jambo unalofanya, hakikisha  kuwa unalifanya kwa bidii huku akili na nguvu zako zikiwa kwa asilimia  95, ukifanya hivyo lazima utapata mafanikio.
Baada ya kuwa na  bidii kwa kiwango hicho, jambo linalofuata ni uaminifu wako katika  mazingira unayofanyia kazi. Kumbuka kuwa uaminifu haujali kama wewe ni  mfanyakazi au mfanyabiashara bali kwa kila eneo unalofanyia kazi  hakikisha kuwa unakuwa muaminifu kwa kiwango kikubwa. Uaminifu katika  kazi zako lakini pia uaminifu kwenye mali za wengine.
Mathalani  bosi wako amekuagiza kufanya jambo linalohitaji fedha nyingi, basi  usifanye ujanja wowote kuzidisha kiwango cha kawaida kwani kufanya hivyo  si ujanja badala yake ni kujiwekea mazingira magumu sana maishani.
Hivyo uanimifu ni nguzo nyingine muhimu sana katika safari ya kutafuta mafanikio maishani mwako.
Unapokopa  fedha au kitu flani kwa mtu, hakikisha unakirejesha kwa muda  mliokubaliana, achana na tabia ya kudhulumu vitu ambavyo si halali kwako  kwani utafiti wa kisaikolojia unaonesha kuwa, mali zote zinazopatikana  kwa njia za mkato au njia ambazo si za uaminifu mara nyingi huwa  hazidumu.
Hivyo msomaji wangu, jitahidi sana kuboresha eneo la uaminifu katika mazingira unayojipatia riziki maishani mwako.
Lakini  pia, nguzo nyingine ni Ukweli kwani ukitaka kuishi maisha ya amani na  yenye furaha basi jitahidi sana kusema ukweli kwa kila sentensi  inayotoka kinywani mwako. Katika ofisi ninayofanyia kazi, ninashika  nafasi ndogo sana ya uongozi lakini kitu ambacho huwa nasisitiza kwa  wafanyakazi wenzangu ni kusema ukweli.
Achana na ahadi ambazo  unajua kabisa kwamba huwezi kuzitimiza kwani ukijijengea mazingiara ya  uongo katika jamii unayoishi basi utakuwa unafukuza myanya ya mafanikio  maana unaweza kuwa na kitu cha muhimu sana kukifanya lakini kwa kuwa  umejijengea  mazingira ya uongo basi hakuna atakaye kuamini.
Ukiwa msemakweli, hautalaumiwa na mtu na wala hutamlaumu mtu.
Mfano,  rafiki yako anakuomba umfanyie jambo flani kwa wakati maalum na wewe  unakubali japo unakuwa na uwezo mdogo kufanya hivyo, unafikiri kama  muda  ukifika na haujafanya kitu hicho ni nini kitafuata? Jibu ni lawama  kwani umeahidi kitu ambacho huwezi kukifanya na siku nyingine hawezi  kukuamini.
Juu ya hayo yote kuna kitu muhimu zaidi ambacho ni Imani.
Hapa  ndipo kwenye kiini kikubwa cha mafanikio maishani kwani hata kama  unafanya kazi kwa bidii kiasi gani, ni mkweli kwa kiasi gani lakini kama  hauna imani na unachokitaka basi ni vigumu kufanikiwa.
Saturday, March 17, 2012
Nguzo Kuu za Mafanikio Maishani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment