Saturday, March 17, 2012

Hasira na chimbuko lake I

Na kwa hivyo wengine hujikuta wanajiumiza na kutojitendea haki wao wenyewe. Tunapokasirika kupitiliza (ove-react) hasira zetu zina hama mikononi mwetu, zinaanza kutuendesha sisi, siyo sisi kuziendesha hasira hizo, hapafujo hujitokeza, majeraha na maumivu pia hudhihirika. Maumivu haya ya nje ya mwili sikitu, ukilinganisha na maumivu ya ndani yanayosababishwa na kuimeza hasira au kujihukumu kutokana na hasira zetu.

Ukweli kuhusu hasira

Yawezekana umeijua na kuizungumzia hasira kwa muda mrefu lakini hujajua kweli inayohusu hasira na yamkini kweli hii ikawa tofauti na kile ulichokifahamu kuhusu hasira. Hasira siyo tatizo na wala siyo hisia kuu bali ni dalili tu ya kitu kinachoendelea ndani ya mtu. Kuionyesha au kuiachilia hasira yako kwa umpendae au mhusika yeyote hakuipunguzi hasira ile bali kuipalia makaa ili iwake vizuri.

Jinsi tunavyoitumia hasira yetu ni kitu kinachotakiwa kujifunza, hii inamaanisha unaweza ukajifunza njia au namna mpya zakukabiliana na hasira yako na hivyo kuiweza na siyo yenyewe ikuweze wewe. Mwenzako au mpenzi wako hawajibiki kwa chochote katika kukukasirisha, bali wewe unawajibika.

Unajisikia vipi baada ya kuufahamu ukweli huu? Kumbuka kuwa, utendaji kazi wa haya unayoyopata hapa utakusaidia sana katika kuongeza kiwango cha amani na utoshelevu katika uhusiano na maisha yako kwa ujumla.

Nini mizizi ya hasira?

Hasira ni kile kitu tunachokiita hisia ya upili (Secondary emotion) siyo hisia ambazo ndiyo msingi au za kwanza.
Ni mchakato mzima wakutuma ujumbe kukuambia kwamba, kuna kitu kinaendelea ndani yako.
Hasira husababishwa na hofu, maumivu au kuchanganyikiwa.

Hofu:
Unaweza kuwa na hofu kwa mpenzi wako atakuzidi nguvu, uwezo au sauti, unaogopa kupelekeshwa au kutawaliwa, unaogopa kudharauliwa au kutoheshimika, basi kwakujilinda na hofu hii unajikuta unawaka hasira.
Wakati wowote unapojihisi kuwa na hasira jiulize, je kuna kitu ninachokiogopa? Hofu yangu ni nini? Hisia zangu zikoje? Usihofu kumwambia mpenzi wako unavyohisi hofu fulani, na kujua kama je yuko tayari mliongelee? Mwambie ni bora mliongelee kuliko ujikute unakarisika.

Maumivu:
Maumivu haya hutoka kona nyingi sana, kwa mfano, mpenzi wako anakwambia neno kali usilolitarajia kutoka kinywani mwake, au unapika chakula kizuri kilichokugharimu muda halafu uliyemwandalia asije, au asile au wala asiseme kitu baada ya kula chakula hicho, unafanya kazi muhimu kubwa na nzito na hata hupokei pongezi toka kwa yeyote, unaweza kuwa umepigwa na unayempenda, au unaweza kugundua kuwa mpenzi wako siyo mwaminifu, na mengine mengi yanayo weza kuleta maumivu.

Ili kuyapenyeza nje maumivu yetu, tunaamua kuwa na hasira, tunataka mtu mwingine alipe kwa maumivu yanayotupata, tunatamani kuweka ushindi sawa, umeniumiza! na mimi lazima niziumize hasia zako, lakini tunasahau kuwa kwa kumuumiza mtu mwingine hatuleti usawa tunaoutafuta. Tunapoumizwa hatutaki kukubali uzito wa maumivu yale kinyume chake tunaufunika kwa hasira.

Ukijiona umekasirika, jiulize je ninamaumivu yoyote ndani yangu? Je, maumivu haya yanatoka wapi? Kinyume na hasira zako, jaribu kumweleza mpenzi wako kuwa unajisikia kuumizwa

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment