Saturday, March 17, 2012

Hatua 15 za kuondoa mawazo yanayoumiza II


SABA: Namna nyingine ya kukabiliana na mawazo ya kuumiza ni kupunguza hasira juu ya watu wengine. Katika hali ya kawaida matukio mengi husababishwa na watu, kumkasirikia mtu aliyekusaliti, aliyekufilisi, anayekuroga ni adhabu nyingine kubwa unayojipa mwenyewe, hivyo ili ufanikiwe kuondokana na msongo wa mawazo ni vema ukawa mtu wa kusamehe na kutokuwa na hasira na watu wengine ambao unadhani ndiyo chanzo cha tatizo lako.


NANE: Unapokuwa na mawazo yanayoumiza na baadaye ukafanikiwa kuyaacha usikubali kuyarudia tena, lakini watu wengi wanaoumizwa na mambo fulani huwa hodari sana kuyatunza akilini mwao na kuyarejea kila mara, jambo ambalo huwafanya waumizwe na mawazo hayo kwa muda mrefu bila kupumzika. Yametokea, yamepita achana nayo usikubali akili yako iyarejee tena.
TISA: Ikiwa umekuwa na mawazo ya kuumiza kwa muda mrefu, kwa sababu umefeli mtihani au umeshindwa kufanya jambo fulani, mtu kakuudhi, hebu badili mawazo hayo ya kushindwa na ufikirie kushinda katika siku za usoni.

Kwa mfano kama hujazaa mtoto na ungependa kuwa naye, onja furaha hiyo kwa kusema mwaka ujao utampata mtoto. Hatua hii itakusaidia kuitumikiwa furaha hata kama katika hali ya kawaida hujaipata na hivyo kusogeza mafanikio yako karibu zaidi.

KUMI: Yapo baadhi ya mambo ya kuhuzunisha ambayo hutukumba bila kutarajia na hivyo kutuletea mawazo. Njia pekee ya kuyaepuka mawazo ya aina hii ni pamoja na kukubali tukio husika.
Wengi wetu tunapofiwa kwa mfano huwa hatukubali kuamini kilichotokea, matokeo yake ni kuumia kwa muda mrefu. Unapokuwa na tatizo, kwanza likubali kuwa limekupata kisha chukua hatuza za kufaa kulikabili.
KUMI NA MOJA: Msongo wa mawazo unapokuvamia unatakiwa wakati mwingine uchukue hatua za kujipumzisha sehemu tulivu, likiwepo suala la kulala kama inawezekana. Hatua hii itasaidia kuupumzisha mwili na akili kiasi cha kuufanya upate nguvu ya kukabiliana na tatizo.

Hushauriwi kuchukua hatua unapokuwa na msongo mkali wa mawazo. Kama mtu amekuudhi, achana naye nenda kajipumzishe, kesho utajikuta umepata nguvu ya kumpuuza na kuachana naye kabisa.
KUMI NA MBILI: Wakati mwingine kujua sababu zilizoleta tatizo ni muhimu na kwamba hupunguza msongo wa mawazo. Hivyo unapokuwa na jambo ambalo linaikera akili yako, jaribu kutafuta chanzo chake, inawezekana taarifa za mkeo kukusaliti zinazokuvuruga si sahihi, ukiupata ukweli hasa, unaweza kubadili mawazo yako na kupata nafuu ya maumivu.

KUMI NA TATU: Watu wengi wanapopata matatizo ambayo huwatumbukiza katika mawazo mabaya huwa hawako tayari kulipa gharama za kuyamaliza, matokeo yake hubaki wakihuzunika. Kwa mfano mtu anaweza kuwa anadaiwa, mdai wake akamfuata na kumtolea lugha za matusi, jambo la ajabu mdaiwa badala ya kujituma kuhakikisha analipa deni ili ajikomboe anabaki kuhuzunikia matusi. Unapokuwa na tatizo jitume kulimaliza kwa gharama yoyote ili uwe huru, usikae kulia tu bila kupata ufumbuzi wa tatizo.

KUMI NA NNE: Njia nyingine ya kuondokana na mawazo mabaya ni kuyakataa, kwa kufanya kitu kingine ambacho kitakufanya usiwaze matatizo. Tatizo linalowakabili watu mpaka wanashindwa kuyaondoa mawazo mabaya ni kutokuwa na vitu vingine vya kufanya au kufikiri. Msomaji wangu unapojikuta umezama kwenye mawazo yanayoumiza, bila kuchelewa chukua hatua za kuyakataa kwa kuingiza vitu vingine akilini na kuanza kuviwaza, fanya kazi, soma vitabu fanya mazoezi. Epuka pia upweke.
KUMI NA TANO: Tabia ya kukuza mambo kupitia mawazo yetu ndiyo huchangia sana kuwa na mawazo ya kuumiza kwa muda mrefu, inashauriwa kuwa mtu akipatwa na tatizo asilikuze kiasi cha kuliona ni kubwa, asilostahili kulipata na kulifanya kuwa la tofauti kwenye mawazo yake.

Ifahamike kuwa hakuna jambo baya kwa asili, ukiwepo ubaya ni mawazo ya mtu mwenyewe. Dunia ni kioo, ukicheka nayo itacheka ukinuna itanuna. Kwa maana hiyo ukiliwaza tatizo kwa ukubwa litakuwa kubwa, ukilipunguza katika mawazo na kuliona ni la kawaida nalo litakuwa hivyo.
Jambo la mwisho katika somo hili tunalipata kutoka kwa Sir John Templeton ambaye alikuwa na kawaida ya kuwauliza watu ‘what the definition of wealth?’ (Nini maana ya mafanikio ?) ambapo mwenyewe alikuwa anawajibu ‘Live with an attitude of gratitude’ (Ishi katika mtazamo wenye shukrani”.
Kwa kuhitimisha ili mtu aweze kuondokana na mawazo yenye kuumiza ni lazima awe mwenye kupokea kila jambo

Related Posts by Categories



No comments:

Post a Comment