Wengi wamekuwa  wakiumia sana mioyo yao kutokana na ama kukosa penzi la kweli au kuingia  katika penzi la kitapeli wakiamini ni penzi la dhati. Tatizo hili  limekuwa likiwasumbua wengi, inawezekana hata wewe unayesoma makala  haya, limewahi kukukuta au upo katika tatizo hili hivi sasa.
Tatizo  hili husababishwa na kukosa umakini ikiwa ni pamoja na kutofuata  taratibu sahihi kabla na baada ya kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Hapa  sasa ndiyo chanzo cha matatizo. Wapendwa wasomaji wangu, unapokuwa na  simanzi ni wazi kwamba kila kitu kitakuwa hakiendi sawa, maisha  yanabadilika, kila unachokipanga kinavurugika, ufanisi wako kazini  unashuka. 
Siyo ajabu, bosi wako anafikiria kukufukuza kazi  kutokana na kuboronga ofisini. Kimsingi simanzi ni tatizo sugu katika  maisha ya kiuhusiano na ni vyema ikiwa umejifunza mapema jinsi ya  kuepuka simanzi katika maisha yako ya kimapenzi.
Kuna mambo mengi  ambayo wengi huyakwepa ama kwa kuyajua na wakati mwingine bila kujua  kuwa wanakosea na mwisho wanajisababishia simanzi ya moyo.
Katika  mada hii nitakupa dawa ya kukuondolea simanzi moyoni mwako. Inawezekana  umeshakata tamaa, baada ya kuachwa na kila mwanaume unayeanzisha naye  uhusiano ukiamini una mikosi, hapo utakuwa unakosea sana, huna balaa  wala nuksi ndugu yangu, ni kutojipanga na kutokuwa na utayari wa  kukutana na matatizo katika uhusiano.
Hata hivyo, kwa kupitia  mada hii kwa makini utaingiza kitu kipya ubongoni mwako na kukufanya uwe  mpya katika ulimwengu wa mapenzi.
Kuna wengine wamekuwa wakilia  kila siku, inawezekana hata wewe unayesoma mada hii hivi sasa upo katika  matatizo makubwa ya kimapenzi na huoni kama kuna sababu ya kuendelea  kuishi.
Hapo unakosea sana ndugu yangu, maisha bado yanaendelea,  unachotakiwa kufanya ni kujiweka tayari kukabiliana na matatizo yajayo,  huku ukihakikisha kwamba huruhusu matatizo ya kujitakia katika maisha  yako.
Vipo vipengele vingi sana ambavyo kwa kuvifuatilia kwa  makini utaweza kuondoka katika utumwa wa mapenzi unaousumbua moyo wako  na kuharibu taratibu za maisha yako.
KABLA HUJAANZISHA UHUSIANO
Kipengele  hiki kinawahusu wale ambao bado hawajaingia katika uhusiano. Hapa  nitafafanua mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuzingatia kabla ya kuingia  katika uhusiano utakaokusababishia matatizo. Hutakiwi kuwa chanzo cha  matatizo rafiki yangu.
Hapa ni muhimu sana kwako wewe ambaye  unatarajia kuingia katika uhusiano mpya. Umuhimu wake unatokana na  ukweli kwamba, baada ya kugundua vitu vya kuepuka kabla ya kuingia  katika uhusiano itakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuingia katika  uhusiano mzuri, wenye mwanga mbele yako.
(i) Tafakari...
Simanzi  huletwa na mateso ambayo mhusika huyapata akiwa katika uhusiano ambao  hakuutarajia. Hii inamaanisha kwamba ama mpenzi uliyenaye hakupendi au  wewe mwenyewe umegundua kwamba humpendi!
Hisia hizi zinatosha kabisa  kukuingiza katika simanzi ya moyo. Kugundua kwamba mpenzi uliyenaye  hakupendi kwa dhati ni tatizo kubwa sana, maana hapa lazima ataanza  kukufanyia vitimbi na kukukosesha raha.
Kitendo cha kuanza  kumfikiria au kuwaza juu ya mabaya anayokufanyia ni mwanzo wa wewe  kufanya vibaya kazini, kutojijali, kupoteza hamu ya kula na mwisho hata  afya yako itakuwa ya mashaka.
Katika kukabiliana na hili ni  lazima ufikirie zaidi kabla ya kuingia katika uhusiano na patna mpya.  Ukiondoa suala la yeye kukupenda, jiulize je, unampenda? Ni kweli moyo  wako umeridhika naye?
Saturday, March 17, 2012
Hivi anakutesa au unajitesa mwenyewe?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment