Niseme  kwamba mapenzi ni idara ambayo ukiipatia, maisha yako yatakuwa  ni ya furaha sana na utatamani kifo kisiwepo ili uishi milele lakini  ukikosea kidogo tu unaweza kujikuta ni mtu wa kulia kila siku na wakati  mwingine kujuta kwa nini Mungu alikuleta duniani.
 
 Ndiyo maana huwa nasema, fanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mtu sahihi  ambaye moyo wako unaamini atakupata furaha uliyoitarajia. 
Baada ya kumpata mtu huyo, tumia gharama yoyote kumshika vilivyo ili  asikuponyoke. Hakikisha unamfanya akuone wewe ni wewe na bila wewe  maisha yake hayajakamilika.
Hilo litawezekana kama tu utamjali kwa mambo muhimu ambayo nimekuwa  nikiyaandika mara kwa mara kupitia safu hii. Sina sababu ya kuyarudia  lakini leo nataka kugusia mambo matatu ambayo baadhi ya watu wamekuwa  wakiyapotezea na mwishowe kujikuta wanayachukia mapenzi kwa sababu za  kujitakia.
Ukijaribu kufuatilia kwa karibu utabaini kuwa, wapo wanawake ambao  wamekuwa wakijitengenezea mazingira ya kusalitiwa bila kujua.
Wapo ambao hawajui nini wawape wapenzi wao ili kuwadatisha, wapo ambao  wanajua wanachostahili kuwapa wapenzi wao ila kwa makusudi tu wanaamua  kutowapa lakini baadaye wakitemwa wanaanza kulia.
Wanaume wanapenda vitu adimu kutoka kwa wapenzi wao, wanapenda vitu  ambavyo wanahisi wenzao hawawezi kuvipata kutoka kwa wapenzi wao. Hivyo  ndivyo unavyotakiwa kumpa mpenzi wako ili uweze kumshika.
Ninaposema hivyo simaanishi kwamba unatakiwa kumpa mpenzi wako mapenzi  kinyume na maumbile, maana najua wapo ambao wameelekeza mawazo yao huko. 
Chondechonde simaanishi hayo jamani.Tena naomba niseme kwamba wanaowapa  wapenzi wao mapenzi kinyume na maumbile hawajipendi, wanayachukia maisha  yao na wako tayari kwa lolote. Sikushauri kabisa ufanye hivyo kwani ni  hatari kwa maisha yako.
Ninaposema umpe mpenzi wako kile ambacho wengine hawawapi wapenzi wao namaanisha mengi lakini haya yafuatayo ni ya msingi;
Utundu na ubunifu
Mapenzi ni utundu na ubunifu hasa unapokuwa kwenye uwanja wa sita kwa  sita na mtu uliyetokea kumpenda sana. Onyesha utundu wako wote, tumia  akili yako kubuni vitu ambavyo unaamini vitampagawisha mpenzi wako. Kwa  kufanya hivyo unaweza kuwa wa kipekee kwake na ataamini amempata mtu  sahihi.
Usimbanie
Katika hili naomba niseme kwamba mapenzi ni sawa na chakula. Mwanamke  anayempenda mume wake anatakiwa kuhakikisha anampa chakula pale  anaposikia njaa. Tena mwanamke huyo atampa chakula kwenye ‘hot pot’  kikiwa cha moto na mume atajisevia kiasi kinachomtosha.
Kwenye mapenzi nako ni hivyo hivyo. Mpenzi wako akihitaji kuwa na wewe  faragha usitoe visingizio visivyo na msingi na muwapo faragha mpe uhuru  wa kula apendavyo, kwa staili aitakayo ila hakikisha unamzuia asile  ‘makoko’ kwani yana madhara kwake na kwako.
Kama utafikia hatua ya kumpa mpenzi wako mapenzi kwa ratiba au kumpa  penzi katika mazingira ya kigoigoi, tambua siku zako za kuachwa  zinahesabika.
 Maneno matamu
Mumeo ni mtu wa kumpa maneno matamu kila wakati, maneno ambayo  yatamfanya ajisikie kuwa pembeni yako kila wakati.Wapo wanawake ambao  hawako makini katika hili na kujikuta ni watu wa kubwatuka ovyo.
Waswahili wanasema maneno matamu ni silaha katika maisha ya kimapenzi hivyo chuja ya kumwambia mtu wako.
No comments:
Post a Comment