Kuna kitu kimoja ambacho naamini masikio huwa yanasikia hata macho  kuona, lakini moyo siku zote huwa haukubali. Leo tuuandae moyo  kukubaliana na jambo ambalo huamini kuwa haliwezekani:
Ni jambo gani?
Jambo  hilo ni kuachwa. Katika uhusiano wa kimapenzi ambao siyo rasmi, kuna  matukio mengi ambayo huwafanya baadhi ya watu kusikia kauli lakini moyo  usikubali.
Ni kauli gani?
Kuna walioniuliza kuwa inapotokea  mmoja katika uhusiano anamweleza mwenzake: “Mimi na wewe mapenzi basi.”  Je, atajuaje kama mtamkaji anamaanisha?
Ukitaka kujua kama  anamaanisha utaona mawasiliano hasa ya simu yanakuwa ya shida tofauti na  zamani. Hataonyesha ushirikiano na hata ukitaka kujua sababu majibu  yake yanakuwa ya kiburi.
Wengi wanateseka sana kufikia hatua ya  kuchanganyikiwa kutokana na wapenzi wao kutowaeleza sababu za msingi za  kuvunjika kwa penzi lao.
Kwa kawaida mtu akikuambia ‘sikutaki’ na  akiwa anamaanisha, unatakiwa kuachana naye, lakini kwa udhaifu wa  wanadamu tuna tabia ya kubembeleza ili kuhakikisha tunayamaliza na  kurudi katika hali ya kawaida.
Kwa vile penzi lenu halikuwa na macho, anayelivunja kuna kitu alijiandaa zamani ndiyo maana hakuonei huruma.
Nini cha kufanya?
Kama  amekueleza ‘hakutaki’ lakini bado ukafanya bidii ya kumbembeleza na  ikashindikana, ilihali macho yameona, masikio yamesikia, inabidi  kukubaliana na kilichotokea hata kama ulimpenda. Kumbuka hakuwa abiria  katika safari ya maisha yako.
Moyo utakubali?
Unatakiwa ujifahamu wewe ni nani na kutambua kuwa kumpata mpenzi wako haikuwa kama kuokota kitu.
Kama nilivyowahi kusema kuwa mapenzi ni bahati, elewa uliyemchagua au aliyekuchagua hakuwa bahati yako.
Ukishafahamu  hilo, fanya kama mfanyabiashara aliyetegemea faida lakini amepata  hasara ambayo hawezi kuing’ang’ania, bali atabadili mwelekeo.
Penzi  linalokutesa ni biashara ya hasara ambayo ni lazima uibadilishe. Nina  uhakika utampata uliyemkusudia, hakuna aliyeumbwa duniani kuumia milele.
Faraja nyingine zinatafutwa, usikate tamaa, jipange upya, ueleze moyo wako kwamba, aliyepita hakuwa sahihi kwako.
Saturday, March 17, 2012
Penzi linalokutesa ni biashara hasara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment