Je,unakabiliwa  na ugumu katika kutimiza malengo yako kimaisha? Bado hutakiwi kukata   tamaa hata kidogo.
1.KUWA MAHUSUSI NA MALENGO YAKO
Kwanza kabisa katika kuelekea kutimiza malengo yako, unatakiwa kuwa mahususi na unachokitaka.
Lakini pia, ni lazima ujitengee muda maalum wa lini unatakiwa kutimiza lengo hilo.
Usijiwekee malengo yasiyo na mipaka katika kuyatizimiza. Vinginevyo utaishia kuwaza kila kukicha.
Baada ya hapo, yaandike malengo yako kwenye karatasi, kwa kufanya hivyo kunakusaidia kujiweka karibu na malengo yako.
2.JIKUMBUSHE MARA KWA MARA
Hakikisha  kuwa kila siku unajikumbusha juu ya majukumu yako katika kutimiza  malengo hayo. Weka karatasi hiyo mahali ambapo utakuwa unaiona kwa  urahisi kila mara.
Mfano, iweke kwenye kioo chumbani mwako kwani  ni rahisi kuiona na hali hii itakufanya  uzidi kujikumbusha zaidi nini  unatakiwa kufanya.
Au unaweza kuiweka kwenye meza yako  unayofanyia kazi kila mara. Kama nilivyosema hapo awali kuwa, kiini hasa  katika kufanya hivi ni kuzidi kujikumbusha juu ya malengo yako kila  mara. Ni amini, hufanya kazi.
3. JIHAMASISHE KUCHUKUA HATUA
Watu wengi hushindwa kuchukua hatua katika kutimiza ndoto zao kwa sababu hawahamasiki vya kutosha  juu ya malengo yao.
Tafuta  vichocheo madhubuti vitakavyokusaidia kuhamasika na kuchukua hatua za  muhimu, ni lazima lengo litimie. Kwa mfano, labda lengo lako ni kuacha  uvutaji wa sigara na binti yako ndiye hamasa kubwa katika hili, mfikirie  kila unapokuwa unataka kuvuta.
4. JIADHIBU UNAPOSHINDWA, NA JIPONGEZE UNAPOFAULU
Kila  unaposhindwa kuchukua hatua, basi unapaswa kujiadhibu  na jipongeze  unapofanikiwa kutimiza kile ulichojipangia.Hakikisha kuwa kila lengo  unalojiwekea ni lazima uwe na mikakati ya kulitimiza.
Kwa upande  mwingine, unaweza kujiadhibu kwa kuchelewa hata kulala kama hujatimiza  lengo la siku hiyo. Katika kufanya hivyo utajiwekea mazoea akilini na  mwilini kufanya kazi kutokana na jinsi ulivyolenga au kupanga.
5. JIONE KAMA UMETIMIZA LENGO LAKO
Hakikisha kila siku unatumia angalau dakika 15 kufikiri  akilini mwako katika mfumo chanya kuwa umeshalitimiza lengo lako.
Hili  ni zoezi la muhimu sana katika kuelekea kutimiza malengo yako. Kujiweka  kama umeshatimiza Malengo  yako  akilini mwako, utakuwa unazidi  kujihamasisha  na utakuwa unafikisha ujumbe kwenye ulimwengu wa  mafanikio kile unachokitaka maishani.
Watu waliofanikiwa katika  nyanja mbalimbali kimaisha, hufanya hivi kila mara, hutimiza malengo yao  akilini kabla ya uhalisia. Hii ni kanuni ya kitaalamu.
6. CHUKUA ANGALAU HATUA 1 AU 3 KILA SIKU
Inashauriwa kuwa, unapaswa kuchukua angalau hatua moja au tatu kila siku zitakazo kuwezesha kutimiza malengo yako.
Hakuna  kitakachotokea kwako kama hutachukua hatua yoyote. Hapa naomba  nieleweke kuwa, hata kama utatumia  muda mwingi kiasi gani kuangalia  hiyo karatasi yenye malengo yako kila siku, lakini kama hauchukui hatua  yoyote  hakuna kitakachotokea.
Kwa hiyo chukua angalau hatua moja au tatu zitakazo kupeleka katika malengo yako kila siku.
7. JIZATITI KWA WENGINE
 Jaribu kuwaambia baadhi ya watu wako muhimu juu ya malengo yako.
KWANZA kabisa kama ilivyoada nimshukuru Mungu kwa kuweza kunipa nguvu ya  kuandika haya nitakayoandika leo na pia kumuomba atuzidishie amani yetu  hapa nchini.
Bado tunaendelea na mada yetu ambayo tuliianza wiki iliyopita na hapa tunahitimisha kwa hoja zilishoshiba.
Kabla ya kuendelea na makala yetu, naomba nieleze jambo moja muhimu sana maishani.
Unapokuwa  katika harakati za kutimiza ndoto zako, basi vikwazo na vizingiti vingi  sana vitaibuka kwa lengo la kukukatisha tamaa, hata siku moja acha  kabisa tabia ya kukata tamaa.
Siku zote maisha ni magumu hivyo ni lazima upambane nayo kwa silaha ya uvumilivu. Na vikwazo visikuzuie kusonga mbele.
Sasa tuendelee na vipengele vilivyosali.
7. JIZATITI KWA WENGINE.
Jaribu kuwaambia baadhi ya watu wako muhimu juu ya malengo yako.
Uko  siriazi katika kutimiza malengo yako? Kama ni kweli, jizatiti juu ya  malengo hayo. Mwambie kila mtu juu ya kile unachotaka kukitimiza  maishani mako. Mwambie mke wako juu ya malengo yako, waambie wazazi  wako, waambie rafiki na jamaa zako juu ya malengo yako na lini hasa  unapanga kuyatimiza.
Ukifanya hivi, utakuwa huna jinsi zaidi ya  kutimiza malengo yako,  maana umewaabia watu wa muhimu sana hivyo  kushindwa kwako kutimiza malengo hayo, ni sawa na kujiletea aibu kubwa.
Hivyo utachukua hatua siriazi na kujiletea matokeo halisi.
Lakini naomba nitoe angalizo kuwa, simaanishi kwenda mitaani na kuanza kuwatangazia watu wote, namaanisha watu muhimu tu.
8. PIMA MATOKEO YAKE
Pima na jiwekee muono juu ya matokeo yako.
Kamwe  huwezi kujua kama unavuka hatua kuelekea kwenye lengo lako kama hupimi  matokeo ya kile unachokifanya kila siku katika utendaji wako wa kazi.
Kama ukigundua kuwa hauzalishi matokeo unayoyataka, basi huenda huchukui hatua za kutosha, au mikakati unayoitumia siyo sahihi.
Hivyo unapaswa kubadili mikakati katika kujipatia matokeo unayoyataka.
Kama unazalisha matokeo unayoyataka, basi hongera. Chukua hatua zaidi ili ujipatie matokeo zaidi.
9. KUWA NA SABABU.
Ni  lazima uwe na sababu za kwa nini unataka kutimiza lengo hilo maishani  mwako. Ukiwa na lengo lisilo kuwa na sababu mara nyingi huwa ni vigumu  kulitimiza maana hakuna kitu kinachokusukuma katika kufanya hivyo.
Hakikisha unajikumbusha kila mara akilini mwako kuwa ni kwanini unataka kutimiza hilo lengo maishani mwako.
Sababu yako yakinifu ndani ya moyo ni chanzo cha hamasa. Mara zote kumbuka hili.
 
10.JIKUMBUSHE YA JUU.
Ni muhimu sana kujikumbusha yote uliyoyasoma hapo juu.
Utafiti  umaonesha kuwa ukitaka tabia fulani ijekengeke, ni lazima uifanyie  mazoezi kila siku ipitayo angalau ndani ya siku 21mfululizo.
Japo  siyo rahisi mwanzoni. Ni kama tu kuhamia mazingira mapya, unaweza  kujisikia ugumu kidogo, lakini muda si mrefu utazoea maana akili yako  itakuwa imejikita huko.
Ni sawa na hapa. Fanyia mazoezi tabia njema kila siku kwa muda wa siku 21 na tabia hiyo itakuwa yako milele.
Watu  wengi huwa hawajiulizi ni kwa jinsi gani husugua meno yao kila  asubuhi.  Unajua ni kwa jinsi gani unasugua meno yako kila asubuhi?
Bila shaka ni vilevile kama kawaida.
Hivyo ndivyo ninavyomaanisha kitabia. Unapoanzisha tabia mpya, utafanya mambo vilevile kila siku.
Kwa  kufuata njia zote kumi nilizozianisha hapa chini, naamini kwa nguvu  zote kuwa kutimiza  malengo yako haitakuwa tatizo tena.  Fanya hivyo kwa  dhati na utaona matokeo ya kushangaza. Naomba niishie hapa kwa leo.
ZINGATIA HAYA.
Katika  maisha, hakuna kinachoshindikina kama kweli utaamua kwa dhati kukipata.  Kinachochangia watu wengi kutotimiza kile wanachokitaka maishani, ni  kutodhamiria kwa nia na nguvu zote kufuatilia malengo yao. Lakini pia  woga huchangia kwa kiasi kikubwa sana. Kabiliana na hofu. Tunapokuwa  waoga, huwa tuna sizi kiakili, kimwili na kihisia na hushindwa kabisa  kuchukua hatua.
Saturday, March 17, 2012
Njia 10 za kutimiza lengo lako maishani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment