1- Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji  yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo asaidie au atoe.
2 - Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .
3 - Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri .
4 -Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5 – Mpenzi/rafiki wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .
6 – Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule atakayekupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya  shinikizo fulani (pesa au mali)
7 – Mpenzi/rafiki wa kweli  ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine
8  - Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli .
9  -Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
10  - Atakuwa tayari kuvumilia hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia  lugha chafu au ubabe.  Ni hayo tu jipeme na umpime umpendaye!
Thursday, March 15, 2012
Sifa 10 za rafiki wa kweli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment