Kila  kiumbe kina utashi wa kupenda kwa vile upendo ndiyo tuliohimizwa sisi  wanadamu, lakini ukizidi unakuwa ugonjwa ambao huenda usipate dawa. 
  Naleta maada hii baada ya kupata swali kutoka kwa dada yangu mmoja  ambaye alitokea kumpenda kaka mmoja hadi kufikia kushindwa hata  kuzungumza pale anapomuona.
Amejikuta akishindwa kujiamini kujieleza  kwa yule kaka na kuona hawezi kuzungumza chochote kitakachoeleweka kwa  vile amepoteza kujiamini kutokana na kumpenda kupita kiasi.
Kupenda  bila kujielewa ni sawa na wendawazimu, hata unapokuwa ndani ya penzi  hilo lililokutia wendawazimu, unapoteza kujiamini kwa kuogopa kulipoteza  penzi ulilolitafuta kwa muda mrefu.
Nimekuwa nikielezea kujiamini  kwa mwanadamu mbele ya mapenzi na kutojishusha thamani hata kama  umempenda mtu kupindukia. Kupenda ni haki yako ya msingi lakini usiwe  mtumwa wa mapenzi kwa kushindwa kujitambua wewe ni nani na kwa nini upo  pale.
Kupenda sawa, lakini ukizidisha inakuwa sumu inayokutafuna  taratibu kwa vile huna maamuzi yoyote ya moyo wako kwa kuogopa kumuudhi  umpendaye. Hii si kwa wanawake bali kwa watu wote.
Wapo wanaofanyiwa  vituko vya makusudi na wapenzi wao kwa vile tu wanatambua wanapendwa na  kukaa kimya kiasi cha kuwashangaza watu.
Kwa vile hujiamini na  mapenzi ndiyo yaliyochukua nafasi kubwa kwako na kuziba mishipa ya  ufahamu na kuamini hakuna mpenzi mzuri kama uliyenaye na kuona kumpata  kwako ni bahati, unakuwa huna maamuzi, kila utakaloambiwa unaona sawa,  liwe zuri au baya.
Hapa kidogo napenda mnisikilize kwa makini, kila  kiumbe kina haki ya kupenda, lakini lazima ujue unayempenda kama kweli  ana mapenzi ya dhati kwako. Kwa vile unampenda unajitoa kwake kama  kafara ya mapenzi na kuwa tayari kufanyiwa chochote lakini usiachwe.
 Tumeshuhudia wanawake kwa wanaume wakiteseka ndani ya mapenzi yao kwa  penzi la upande mmoja, unayalazimisha mapenzi kwa vile tu unampenda na  kuona hakuna kiumbe chochote mbele yako. Acha kuwa kipofu wa mapenzi,  siku zote mbegu ya upendo huota katika moyo wenye rutuba ya upendo.
 Usihadaike na rangi tamu ya chai sukari, matendo mema ndiyo yanayojenga  upendo ndani ya nyumba. Usiitupe ovyo mbegu yako kwa vile tu umetokea  kumpenda na kwamba kila ukimuona unachanganyikiwa.
Je, unajua  historia yake? Ana mapenzi ya kweli kwako? Jiepushe kuutoa mwili wako  ovyo kwa vile umependa tu bila kujua mwenzako naye anakupenda.
Hata  unayempenda ukimpata basi usikubali kuwa mtumwa wa mapenzi, kwa penzi  kukuongoza wewe na si wewe kuliongoza penzi. Siku zote wewe ndiye  uliongoze penzi na kutoa maamuzi pale litakapokwenda kinyume.
Hii itakufanya uonekane mwenye msimamo na si mtu wa kuburuzwa.
Saturday, March 17, 2012
Usiwe Kipofu wa Mapenzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment