KATIKA mapenzi ya sasa, mahaba ‘chakula cha usiku’ yanapewa nafasi kubwa  sana katika kuleta furaha kwa wawili waliotokea kupendana kwa dhati. 
Asikuambie  mtu, kumnyima mpenzi wako penzi wakati anapolihitaji unamuumiza kuliko  maelezo na anaweza kufikia hatua ya kuhisi humpendi. Atafikiria hivyo  kwa kuwa umemnyima raha aliyotarajia kuipata kutoka kwako.
Hapa  tunatakiwa kufahamu tu kwamba, furaha ya maisha ya binadamu yeyote  inakamilika kwa kuwa na mtu mwenye mapenzi ya dhati kwake na akapatiwa  kila alichotarajia yakiwemo ‘mahabati’.
Katika siku za hivi karibuni  kumeibuka tatizo la baadhi ya wanawake kulia kunyimwa ‘mambo’ na waume  zao. Mfano wa wanawake hao ni Jastina wa Morogoro ambaye anaeleza kuwa,  amefikia hatua ya kutaka kumsaliti mumewe kutokana na kutotimiziwa haki  yake hiyo ya ndoa.
“Mimi ni mwanamke bwana, nina hisia na kuna wakati  najisikia kabisa hamu ya kukutana na mume wangu faragha lakini sasa  mume wangu akirejea nyumbani na nikamwambia kuhusu hilo, anakuwa mkali,  eti kachoka!
“Ingekuwa ni siku moja moja sawa lakini yeye kila siku  akirudi anakula, analala tena anageukia huko… inakuja kweli? Hivi na  mimi nikisema nitafute kidumu changu cha kuniliwaza pale ninapojisikia  nitakuwa nakosea?” alilalamika mama huyo.
Malalamiko haya yanaingia  akilini licha ya kwamba mawazo aliyonayo Jastina ambayo naamini wapo  wengine walio katika mazingira kama hayo siyo sahihi. Mke ana haki ya  kupewa ‘chakula cha usiku’ na kama kuna sababu za msingi ni suala la  wawili kuzungumza na kuafikiana.
Kitendo cha mume kumbania penzi  mkewe kwa maelezo kwamba amechoka kutokana na kazi za kutwa nzima  kinaweza kuchangia usaliti katika ndoa.
Najua katika maisha ya sasa  watu hasa wanaume wanatumia muda mwingi sana kusaka fedha kwa kufanya  kazi na mwisho wake wakirudi nyumbani wanakuwa wamechoka kiasi cha  kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi. Lakini sasa ni sahihi kwa wanandoa  kukaa muda mrefu bila kupeana mambo? Jibu ni hapana!
Kama ni hivyo,  nawashauri wanaume wanapofanya kazi wakumbuke kuna wake zao wapendwa  wanawasubiri nyumbani. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake licha ya  kwamba kazi nayo ina umuhimu wake.
Pia kuna jambo ambalo wanaume na  hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi.  Unapofanya mazoezi unawezesha damu kuzunguka na kufika sehemu zote za  mwili kwa kiwango kinachotakiwa.
Kukaa ofisini kutwa nzima na kurudi  nyumbani na kukaa kwenye kochi kisha kuangalia TV siyo aina ya maisha  inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali  kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa ‘chakula cha usiku’ na kukipokea  huwa kubwa.
Lakini wanawake nao kuna wanaoishi kizamani sana. Hawa  ni wale wanaosubiri waume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata  mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati ‘chakula cha usiku’.
Saturday, March 17, 2012
WANAUME TUSIWALAZIMISHE WAKE ZETU KUWA NA ‘VIDUMU’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment